title : Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate
kiungo : Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate
Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate
Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia umetoa msaada wa vitabu vya ziada 285 kwa wanafunzi 200 wa Shule ya Sekondari Bugisha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za mgodi huo kusaidia maendeleo ya elimu nchini.Msaada huo ni sehemu ya ufadhili ndani ya programu ya CanEducate inayoendeshwa na kampuni hiyo.
CanEducate ilianzishwa mwaka 2010 lengo kuu likiwa ni kudhamini wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika familia maskini. Chini ya programu hiyo, wafanyakazi huchangisha fedha chini ya mfuko maalumu na kisha kampuni ya Acacia hutoa kiwango sawa na kile kilichochangishwa. Fedha hutumika kulipa ada za shule, kununua sare, vitabu na vifaa vya shule kwa wanafunzi.
Wakati wa kuanzishwa kwake, mpango huo uliwasaidia wanafunzi 158 walio karibu na Mgodi wa Dhahabu ya Bulyanhulu. Hata hivyo, kutokana muitikio mkubwa kutoka kwa wafanyakazi na makandarasi wa Acacia, programu imeweza kukua zaidi na kuwafikia zaidi ya wanafunzi 800 kutoka shule zinazoizunguka Buzwagi.
Moja ya sababu ambazo zinachangia kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita, ni ukosefu wa vitabu mashuleni, na gharama za vitabu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kifedha wa wazazi na walezi.
Katika eneo la Buzwagi, mpango huo unahusisha shule tatu za sekondari; Shule ya Sekondari ya Bugisha, Shule ya Sekondari ya Mwendakulima, na Shule ya Sekondari ya Nyasubi ambazo zimetoa wanafunzi bora katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita.
Msaada uliotolewa kwa Shule ya Sekondari ya Bugisha ulisimamiwa na maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa Buzwagi, Yunia Wangoya na Antonia Kiondo.
Msaada huo ulitolewa mbele ya walimu, wazazi na wanafunzi ambao kwa pamoja walitoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya Acacia kwa kuwezesha upatikanaji wa msaada huo mkubwa.
Hivyo makala Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate
yaani makala yote Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/shangwe-zatawala-wanafunzi-wakipokea.html
0 Response to "Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate"
Post a Comment