title : MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI
kiungo : MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI
MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI
Jiji la Mwanza limepima viwanja 24,000. Ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kuondokana na Makazi Holela katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Akizungumzia mafanikio hayo hivi karibuni; Mratibu wa masuala ya Urasimishaji, jijini Mwanza, ambaye ni Afisa Mipango Miji; Athuman. S. Simba alisema; “Katika kufanikisha utekelezaji uliofanyika; Halmashauri ya Jiji iliunda vikosi kazi vipatavyo kumi na tatu (13) na kuvipangia majukumu mbalimbali. Vikosi kazi hivyo vilifanya kazi za uandaaji wa michoro ya mipangomiji, upimaji, ukaguzi wa viwanja na kumilikisha”
Aidha, Katika zoezi zima la upimaji wa viwanja 24,000. Taarifa yake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza; Hosiana B. Kusiga; imesema kuwa; Viwanja 19417 vimepimwa (Approved), maeneo ya Kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, na Nyegezi. Vile vile, Viwanja 5515 vimefanyiwa upimaji wa awali (Dermation).
Kazi ya upimaji inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Mkolani, Lwahnima, Igoma, Mhandu, Kishiri na Luchelele. Ambapo Idadi ya viwanja vilivyokamilika na vilivyo kwenye upimaji wa awali (demarcation) jumla yake ni 25,032. Utekelezaji wa upimaji huu ni kutoka kwa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mhe. William Lukuvi, kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuandaa Hati Miliki za viwanja 35,000 kupitia mradi wa urasimishaji makazi holela .
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo Ukuta unaoonekana pichani unategemewa kuondolewa kupisha utengenezwaji wa barabara za Mitaa.
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo beckon zimekuwa zikiwekwa katika viwanja.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipuli, Kata ya Mahina; Rajabu Jumanne (mwenye shati la bluu) akishuhudia zoezi la upimaji linavyoendelea katika Mtaa wake, likiongozwa na Mratibu/ Mpima; Yohana Cleophace wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Muonekano wa Barabara iliyochongwa rasmi na Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la Urasimishaji katika kata ya Ipuli, Mahina.
Hivyo makala MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI
yaani makala yote MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/makazi-holela-jijini-mwanza-yaanza.html
0 Response to "MAKAZI HOLELA JIJINI MWANZA YAANZA KUONDOLEWA KWA KASI"
Post a Comment