Rais Dk Shein ateua Majaji wapya

Rais Dk Shein ateua Majaji wapya - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Dk Shein ateua Majaji wapya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Dk Shein ateua Majaji wapya
kiungo : Rais Dk Shein ateua Majaji wapya

soma pia


Rais Dk Shein ateua Majaji wapya


Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Aziza Iddi Suweid kuwa majaji wa Mahakama hiyo.

Pia, amemteua Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa uwezo wake chini ya Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 4 ya 2015, kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya 2017, Kifungu cha 10(a)(1).

Katika uteuzi mwingine, Rais Shein amemteua George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.

Dk Shein chini ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.

Taarifa ya uteuzi huo imesema ulianza jana Ijumaa.


Hivyo makala Rais Dk Shein ateua Majaji wapya

yaani makala yote Rais Dk Shein ateua Majaji wapya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Dk Shein ateua Majaji wapya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/rais-dk-shein-ateua-majaji-wapya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Dk Shein ateua Majaji wapya"

Post a Comment