MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA
kiungo : MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

soma pia


MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

Kwa mara nyingine mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, mchezo unaojinyakulia umaarufu mkubwa nchini Tanzania, umetangaza mshindi wake wa droo kubwa ya Juma la nane ambaye amejishindia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 60. Mshindi huyu si mwingine bali Bi. Rebecca Amos mkazi wa Yombo Vituka, jijini Dar es Salaam. 

Bi Rebecca, mwenye umri wa miaka 22, ameibuka na ushindi huu mnono katika mchezo uliofanyika Jumapili iliyopita na kurushwa mubashara katika televisheni.

Kufuatia zawadi hii ya iliyotolewa Juma hili na aina ya washindi wanaoibuka, mchezo wa Tatu Mzuka ni dhahiri umeendelea kuleta mageuzi makubwa katika eneo la michezo ya Bahati Nasibu hapa nchini. Hii inatokana na aina ya washindi wanaopatikana na pia uwezo Tatu Mzuka kutoa zawadi za washindi zinazofikia kiasi cha shilingi milioni 2 kila saa kwa saa 24 kwa siku. Ushindi huu unatolewa ilhali kiasi cha kushiriki katika mchezo huu kikiwa ni kuanzia shilingi 500 tu huku droo za kusaka washindi zikifanyika kila saa.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu, Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga alisema; “Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”

  Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu,huku akimtaja Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60,picha shoto ni rafiki wa mshindi wa Tatu Mzuka kwa wiki hii,Agness Swai

Maganga  alisema kuwa Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu, kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”
 Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60 za Tatu Mzuka,akitoa ushuhuda wake kuhusiana na mchezo huo na hatimaye nae kuibuka mshindi wa mamilioni.Rebecca amewaasa watu wengine kucheza mchezo huo kwani mmoja wao anaweza akaibuka mshindi na kubadilisha kabisa mfumo wake wa kimaisha kupitia fedha atakazo kuwa ameshinda 
Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Rebecca Amos ,mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 60,mapema leo jijini Dar.


Hivyo makala MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

yaani makala yote MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/mkazi-wa-yombo-vituka-rebecca-amos.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA"

Post a Comment