title : KUMBUKUMBU
kiungo : KUMBUKUMBU
KUMBUKUMBU
MAREHEMU CASSIUS O. MDAMI
Tangu umetuacha tumetafakari mengi tukidhani umesafiri utarudi lakini kumbe haikuwa hivyo. Kuwa kwako mbali na familia kumetufanya kujifunza mengi kuhusu maisha na kutafakari muda ambao tulikuwa pamoja katika maisha ya hapa duniani wakati wa furaha na uchungu. Unakumbukwa na mke wako Rose na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson.
Umetimiza mwaka sasa tangu umetuacha; pengo lako ni kubwa katika kila kona ya maisha na hata katika Tasnia ya Habari uliyoitumikia katika muda mwingi wa maisha yako kwa kutuonyesha kwa vitendo maana ya kuipenda na kuithamini kazi katika maisha.
Tumekosa simulizi za kusisimua za Utalii wa Ndani, ulichimba na kuchimbua mengi ambayo kama si kwa jitihada zako binafsi tusingeyajua kamwe… tumebaki na msemo wako maarufu “Falsafa ya Ufagio ni Unyenyekevu”.
Faraja yetu ni Mungu aliye Baba wa Yatima na mume wa Wajane (Kutoka 22:22-24). Tunaamini katika Ufufuo na Uzima na siku moja tutafurahi nawe mbinguni (Yohana 11:25-26).
Mungu akupe pumziko la Milele, upumzike kwa Amani - Amina
Hivyo makala KUMBUKUMBU
yaani makala yote KUMBUKUMBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUMBUKUMBU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/kumbukumbu.html
0 Response to "KUMBUKUMBU"
Post a Comment