title : KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA.
kiungo : KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA.
KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA.
Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu mara baada ya kusomewa Mashtaka yanayomkabiri Mahakama hiyo kusema kuwa upelezi wa Kesi yake umekamilika.
Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bunda (CHADEMA), Ester Bulaya akimsindikiza Mbunge wa Kawe. Mara baada ya Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na imesema kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.
Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee akiwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda (CHADEMA) wakiwa wamekaa katika Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu ya matusi inayomkabili, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (39) kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na aMaendeleo (Chadema) umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Kishenyi amedai upelelezi katika kesi hiyo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa huyo maelezo ya awali.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala akisaidiana na mawakili, Jeremiah Ntosebya na Hassan Kiangio, amedai kuwa waliiambia mahakama kuwa watawasilisha mapingamizi ya awali ikiwemo makosa ya kisheria kwenye hati ya mashitaka.
Amedai mapingamizi hayo sio ya kimaandishi bali waliiambia mahakama kwamba watawasilisha mapingamizi hayo, lakini kutokana kesi inavyoenda wameona bora waondoe mapingamizi hayo na kusikiliza kesi ya msingi.
Kibatala amedai watakapotaka kuwasilisha mapingamizi hayo watasema na kwamba kwa sasa wanaona faida ya kisheria ni kusikiliza kesi ya msingi.
Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, mwaka kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Katika kesi ya msingi, Mdee anadaiwa kumtukana Rais Dk John Magufuli kwamba "anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break", kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Hivyo makala KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA.
yaani makala yote KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/kesi-ya-mdee-upelelezi-umekamilika.html
0 Response to "KESI YA MDEE UPELELEZI UMEKAMILIKA."
Post a Comment