title : JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR.
kiungo : JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR.
JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR.
Mwambawahabari
Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwapamoja wametembelea kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili Showroom zote za Magari Dar es Salaam Kigamboni kwaajili ya kujionea Maeneo watakayojenga Kituo cha Polis na Kituo cha Zimamoto.
Upande wa Jeshi la Polisi umewakilishwa na Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamanda Benedict Kitarika ambae amempongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuwapatia eneo la kutosha kwaajili ya kujenga Kituo cha Polisi ili kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Mali zinazoenda kuwekezwa kwenye eneo hilo unakuwepo.
Amesema Ujenzi wa Kituo cha Polisi Utaanza mara moja na kuwatoa hofu ya Usalama kwa wale watakaohamishia Showroom katika eneo hilo.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Brighton Monyo amesema watahakikisha wanaweka Magari ya Zimamoto ya Kutosha na Visima vya kutosha kwenye eneo hilo ikikuhakikisha Majanga ya Moto hayapati nafasi.
Amewahakikishia Usalama wenye Showroom kwakuwa wamejidhatiti ipasavyo kuhakikisha masuala yote ya kiusalama wa mali zao yanazingatiwa kwakuwa wataweka vifaa vyote vya kuzima kudhibiti Moto.
Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliagiza wenye Showroom zote zilizopo jijini Dar es Salaam kuhakikisha zinahamia Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kabla ya January Mosi Mwakani.
Hivyo makala JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR.
yaani makala yote JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/jeshi-la-polisi-na-zimamoto-kujenga.html
0 Response to "JESHI LA POLISI NA ZIMAMOTO KUJENGA VITUO KATIKA ENEO LINALOJENGWA SHOWROOM ZA MAGARI DAR."
Post a Comment