title : DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES
kiungo : DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES
DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Septemba 30,2017 ameweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mbali ya kuweka jiwe la msingi pia ameendesha harambee kwa ajili ya kupata shilingi milioni 200 kwa ajili kukamilisha ujenzi huo,ambapo wazazi na walezi wameshiriki katika harambee hiyo.
Akizungumza katika shule hiyo,Matiro aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule hiyo ambayo imejizolea sifa lukuki kwa utoaji wa elimu bora.
“Shule hii imejizolea sifa nzuri,hii ni miongoni mwa shule bora kabisa nchini,kila mzazi anapenda mtoto wake asome kwenye shule nzuri,ukifika Shinyanga ukauliza shule gani nzuri,utatajiwa shule hii,nimeambiwa siri ya mafanikio haya inatokana na maono na utayari wa wazazi na marafiki kuisaidia shule hii”,alifafanua Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa pili kulia) akiwasili katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures.
Maandishi yakisomeka kwa lugha ya Kiingereza yakiwa na maana ya 'Jiwe la Msingi limewekwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro leo Septemba 30,2017'.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures.
Hivyo makala DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES
yaani makala yote DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/dc-shinyanga-aweka-jiwe-la-msingi-na.html
0 Response to "DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES"
Post a Comment