title : Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi
kiungo : Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi
Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi
Na Mwashungi Tahir Maelezo
JAMII imetakiwa ijenge mazowea ya kufika katika vituo vya afya mara kwa mara kwa kupima afya zao pia kujiunga na vikundi vya kufanyia mazoezi ili kujiepusha na maradhi yasiyoweza kuambukiza.
Akizungumza na vikundi vya mazoezi pamoja na wananchi wa jimbo la Mpendae Mwakilishi wa jimbo hilo Saidi Mohammed Dimwa wakati alipokuwa akiwa katika maadhimisho ya siku maradhi ya moyo duniani.
Alisema hivi sasa takribani duniani kuna wimbi kubwa ya maradhi yasiyoambukiza ikiwemo shindikizo la damu, sukari na moyo hivyo aliwaomba wananchi wajenge tabia ya kufanya mazoezi ili waweze kuepukana na maradhi hayo.
Amewataka jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza ZNCD kuzidi kutoa elimu na kuwashajihisha wananchi kuacha kula sana vyakula vya mafuta na kupendelea zaidi kula matunda na mboga mboga kwa lengo la kulinda afya zao.
Pia amewaomba watu waache tabia ya uvutaji wa sigara , tumbaku pombe na madawa ya kulevya kwani vitu hivi ndio sababu kuu ya kupatikana maradhi hayo.
“Wizara ya Afya tayari imeweka kanuni ya uvutaji wa sigara na tumbaku ambapo hivi sasa inaanza kuifanyia kazi kwa kuchukuliwa hatua wale wanaovuta hadharani”Alisema Dimwa.
Vile vile amewataka wananchi iwapo baada ya kuchunguza afya na kubainika kuwa wamepata maradhi hayo kufika vituo vya afya kwa kupatiwa ushauri na kutumia dawa kwa uangalifu.
Nae msoma risala wa jumuiya hiyo Mkubwa Ibrahim Khamis amesema hivi ssa ongezeko la maradhi yasiyoambukiza Zanzibar yamefikia asilimia 33 hivyo amewahimiza wananchi wawe na uzoefu wa kufanya mazoezi ili kupunguza mwili na kujenga afya zao. .
Sambamba na hayo mwakilishi wa jumuiya ya watoto wenye ugonjwa wa moyo Abdulwahab Moh’d Suleiman amesema zaidi ya watoto 750 wenye maradhi hayo wanatibiwa nje ya nchi .
Alisema uwepo kwa jumuiya hii Zanzibar ni kufikia malengo kwa kutoa mahitaji maalum kwa watoto hao na kufahamu uwepo wa chombo mbadala na kupatiwa mahitaji yao ya lazima katika matibabu.
Ujumbe wa mwaka huu Linda moyo wako kwa kula vyakula bora na kufanya mazoezi .
Hivyo makala Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi
yaani makala yote Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/jamii-yakumbushwa-kupima-afya-mara-kwa.html
0 Response to "Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi"
Post a Comment