title : JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
kiungo : JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Mwambawahabari
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa majengo ya shule Manispaa ya Dodoma
Moja ya nyumba ya walimu iliyojengwa katika shule ya msingi Nzasa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na vyoo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa.
…………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote kukamilisha miradi ya ujenzi wa madarasa, mabweni, vyoo, maabara, na miundombinu mingine ya shule za msingi na sekondari kabla tarehe 30 Novemba mwaka huu.
Jafo aliyasema hayo leo hii alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi hiyo katika shule ya Nzasa na Ihumwa zilizopo katika manispaa ya Dodoma.
Mnamo mwezi Juni serikali ilitoa fedha kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (P4R) sh.bilioni 16 kwa ajili ya miundo mbalimbali kwa shule 63 za sekondari na shule 56 za msingi katika halmashauri mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Hata hivyo bado kuna halmashauri chache zinasuasua kukamilisha ujenzi huo hali iliyomlazimu Naibu Waziri huyo kuagiza halmashauri zote hapa nchini kukamilisha miradi iliyo pangwa katika maeneo yao kabla tarehe hiyo.
Jafo amesema kwamba hataki kusikia au kuona halmashauri yeyote ambayo itakuwa haijakamilisha miradi hiyo kwa kipindi kilichopangwa.
“Hatua kali itachukuliwa kwa yeyote atakayefanya uzembe ambao utasababisha ujenzi huo kutokamilika,”amesema Jafo
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Jafo amelipongeza sana jeshi la wananchi kutoka kikosi cha Ihumwa kwa kushirikiana na manispaa ya Dodoma kwa kufanikisha ujenzi katika shule ya Nzasa na Ihumwa na ameviomba vikosi vingine hapa nchini kuiga mfano huo mzuri ambao umewezesha kukamilisha miundombinu hiyo kwa gharama ndogo.
Jafo anaendelea na ziara zake za kikazi za kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Hivyo makala JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
yaani makala yote JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/jafo-azitaka-halmashauri-kukamilisha_19.html
0 Response to "JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU"
Post a Comment