SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI

SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI
kiungo : SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI

soma pia


SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ametoa onyo kali kwa wale wanaofanya uhalifu kwa njia ya mtandao kuchukua tahadhari kwani hawapo salama na kuahidi kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, katika mkutano uliokutanisha uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Naibu Waziri Ngonyani amesisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamendelea kufanya doria katika mitandao ili kubaini watu ambao wanatumia vibaya mitandao.

“Tutumie mitandao kwa ajili ya kuleta maendeleo na si kinyume chake kwani ukifanya uhalifu wowote kwa njia ya mtandao tutakukamata popote ulipo na kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”, amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi kutumia kikoa cha Tanzania (.tz), na Kituo Mahiri cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao ili zisiingiliwe kwa urahisi na kuweza kuibiwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliokutanisha Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupata elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, Utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari, jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Juma (wa pili kulia), akizungumza na wajumbe wa Kamati na watendaji wa TCRA katika ziara ya kikazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani. 
Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayohusu Sheria ya Usalama wa Mitandao. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari .
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam. 




Hivyo makala SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI

yaani makala yote SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/serikali-kuwashughulikia-wahalifu_24.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU MTANDAONI"

Post a Comment