title : Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki
kiungo : Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki
Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki
Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose Mario Vaz ameahidi kuwa, nchi yake itaridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu (AfCHPR) mapema iwezekanavyo .
Akizungumza na ujumbe wa mahakama hiyo ulioko katika ziara ya kikazi nchini Guinea Bissau, Rais Vaz alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba Guinea Bissau ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za umoja wa Afrika kutia saini itifaki iliyoanzisha AfCHPR mwaka 1998.
Katika mazungumzo yake na ujumbe huo ulioongozwa na rais wa AfCHPR mheshimiwa Jaji Sylvain Ore kiongozi huyo wa Guinea Bissau alielezea kuridhishwa kwake na madhumuni ya kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu na kuongeza kuwa masuala ya haki za binadamu yana umuhimu mkubwa katika kufikiwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi za Afrika na kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini na ufukara.
“Ahadi yangu ni kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu katika nchi yangu” alisisitiza Rais Vaz.
Ujumbe wa AfCHPR pia ulikutana na waziri mkuu wa Guinea Bissau Mheshimiwa Umario Sissoco Embalo ambaye alisema mamlaka husika za nchi yake zitaandaa nyaraka zinazohitajika ili kuzipeleka katika bunge la taifa nchini humo kwa lengo la kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu. Raisi wa Mahakama akitambulisha Jaji Matusse kwa Raisi was Guinea Bissau Ikulu. Kushoto wa pili ni Makamu wa Raisi wa Mahakama Jaji Ben Kioko.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki
yaani makala yote Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/rais-wa-jamhuri-ya-guinea-bissau.html
0 Response to "Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau ameahidi nchi yake itaridhia itifaki"
Post a Comment