title : Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa
kiungo : Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa
Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa
Muda mfupi baada ya Kamati ya Uchauzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kumtangaza, Wallace Karia kuwa ndiye rais mpya wa TFF, rais Shirikisho la soka duniani( FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu zake za pongezi.
Hayo yameelezwa na rais wa TFF, Wallace Karia wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza kwa mara ya kwanza mara baada ya kukalia kiti hicho kilikuwa kimeachwa wazi na Jamal Malinzi.
“Kwanza nipende kumshukuru Mwenyezi mungu kwa kufanikisha yote na washukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa imani mliyo hionyesha kwangu nideni kubwa sana nawaahidi sitawaangusha”, amesema Karia rais wa TFF.
Wallace Karia ameongeza kuwa “Muheshimiwa Waziri na wasaidizi wako nawashukuru kwa kutusaidia katika kipindi hiki kigumu tulichopitia, kutoka FIFA na Caf tunawashukuru kwa uwakilishi wenu na mmesimama na kuangalia zoezi letu hadi kufikia hapa nadhani mtakuwa ni mabalozi wazuri kwa utaratibu ambao tumeufanya na demokrasia ambayo imefanyika hapa kuwa na kupeleka salamu hizi”.
“Lakini pia nipende kuwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu muda mfupi nimeongea na rais wa FIFA, Infantino na ametupongeza kwa maamuzi haya amesema yupo tayari na atashirikiana na sisi kwa maswala yote ya maendeleo katika kuhakikisha tunaendeleza soka letu”.
“Wakati huo huo rais wa Caf, Ahmad Ahmad amepiga simu naye yeye ameeleza hayo hayo na amefurahi sana anamategemeo makubwa katika kuendeleza soka letu sina mengi ya kuongea zaidi ya kuwashukuru lakini nipende kuwaambia tu hii furaha iyende kuwa furaha ya kazi”.
By Hamza Fumo
Hivyo makala Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa
yaani makala yote Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/rais-wa-fifa-azungumza-na-karia-dakika.html
0 Response to "Rais wa FIFA azungumza na Karia dakika chache baada ya kuchaguliwa"
Post a Comment