title : NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06
kiungo : NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06
NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BAADA ya kufanyika kwa makosa wakati wa utengenezaji wa Ngao ya Jamii, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini 'TFF' imetengeneza Ngao mpya kwa ajili ya klabu ya Simba baada ya ile ya awali kukosewa kuandikwa.
Klabu ya Simba ilifanikiwa kushinda katika mchezo wa Ngao ya Jamii August 23, 2017 baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 mahasimu wao Yanga na kukabidhiwa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya kiuandishi.
Ngao ya Jamii ya awali iliyokabidhiwa kwa washindi hao wa mwaka 2017 Simba iliandikwa ‘Community Sheild’ badala ya ‘Community Shield’ kitu ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea TFF kuomba radhi kwa wanafamilia wa mpira wa miguu nchini na kuahidi tukio kama hilo halitojirudia tena.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameionesha Ngao ya Jamii iliyofanyiwa marekebisho itakabidhiwa kwa Simba siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas akionesha Ngao ya Jami mpya iliyofanyiwa marekebisho na tayari kukabidhiwa kwa Klabu ya Simba siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.
Hivyo makala NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06
yaani makala yote NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/ngao-ya-jamii-mpya-ya-simba-iko-tayari.html
0 Response to "NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06"
Post a Comment