title : Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba
kiungo : Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba
Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 28 imefanyika leo, huku mkazi wa Goba, jijini Dar es Salaam, Moses Matagili, akifanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda Sh Milioni 20.
Droo hiyo iliyofanyika jana, ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Akizungumza baada ya kumpata mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa ya kuibuka na mamilioni kwa kucheza Biko inayotoa ushindi wenye fursa ya kiuchumi.
Kajala Masanja Balozi wa Biko Tanzania. |
“Tunampongeza mshindi wetu wa droo ya 28, Matagili kwa kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza Biko ili waweze kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwetu.
“Jinsi ya kucheza ni rahisi maana bahati nasibu yetu inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,”Alisema.
Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema mchezo wa Biko unachezwa kwa kufuata sheria zilizowekwa, jambo linaloongeza ufanisi kwa Watanzania wote kucheza na kushinda zawadi za Biko.
“Tunawakumbusha Watanzania kuwa Biko ni mchezo rahisi na ambao unachezeshwa kwa uangalizi mkubwa wa bodi yetu, hivyo kwa wale wanaocheza waelewe kuwa huu ni mhcezo salama,” Alisema.
Wakati Matagili akiibuka kidedea kwa kuzoa Sh Milioni 20 kutoka Biko huku akitarajiwakukabidhiwa fedha zake mapema iwezekanavyo, tayari mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi wa Irnga, akiwa ameshapokea fedha zake Jumatatu iliyopita.
Hivyo makala Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba
yaani makala yote Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/milioni-20-za-biko-zamfikia-moses.html
0 Response to "Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba"
Post a Comment