MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS

MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS
kiungo : MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS

soma pia


MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS

Nahodha wa timu ya Mchenga Mohamed Yusuph (jezi 10) akiwa amerusha mpira ulioleleka langoni mwa timu ya TMT katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Michuano ya Sprite BBall King.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.



Timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars imeanza vyema katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Sprite BBall kings kwa kuweza kuibuka na ushindi wa alama 101 dhidi ya 71 vya TMT.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ulikuwa wa kasi kwa kila upande kwa timu ya TMT Kuonekana kuwabana na kuwalinda Mchenga Bball stars.

Katika mchezo huo wa kwanza wa fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,Mchenga wameweza kuibuka na ushindi wa alama 101 ambapo katika robo ya kwanza na ya pili walionekana kupewa ulinzi mkali na timu ya TMT lakini utulivu, umakini na nidhamu ya wachezaji wa Mchenga uliweza kubadili matokeo katika robo ya tatu na ya nne.
Nahodha wa timu ya TMT Isihaka Masoud amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa fainali ila bado kuna mechi zingine zinazoweza kuamua matokeo na zaidi wanaenda kuangalia wapi wamekosea ili katika mchezo wa pili wa fainali waweze kuibuka kushinda.

"Tunaenda kuangalia wapi tumekosea, turekebishe na katika mchezo wa pili wa fainali tunataka kuhakikisha tunatoka na ushindi kwani mecho moja haiwezi kuamua matokeo ya mechi zilizobaki," amesema Isihaka.

Fainali hiyo inayoendelea katika viwanja vya Don Bosco iliweza kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo pamoja na kutoa Burdani kwa mashabiki wa mpira wa kikapu waliojitokeza kushabikia timu hizi mbili za Mchenga BBall Stars na TMT zote zikitokea Upanga.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja na Young D, Lulu diva, Tammy the baddest, Country Boy ,Kajala, DJ choka na wengine wengi.

Mchezo wa pili wa  fainali utapigwa tena Kesho, Jumatano katika Viwanja vya Don Bosco ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha milion 10, mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa michuano (MVP) atajinyakulia milioni 2.


Hivyo makala MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS

yaani makala yote MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/mchenga-bball-stars-yaanza-vyema.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMA FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS"

Post a Comment