title : MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
kiungo : MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.
Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.
Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi
Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkaziilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.
Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/makamu-wa-rais-awataka-wakazi-wa.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA"
Post a Comment