KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)

KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263) - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)
kiungo : KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)

soma pia


KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)

 Mhandisi Mshauri wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), Eng. Leornado Licari, akitoa maelezo ya mradi wa barabara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatafuta eneo la kujenga kituo cha mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito katika barabara ya Dodoma- Babati (km 263), inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Akizungumza katika eneo la Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji uwepo wa mizani kwa haraka ili kudhibiti  magari yanayozidisha uzito na kuharibu barabara. 

"Hakikisheni mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya miezi miwilli ambapo wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu kumtumia mmoja wa wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka, uwepo wa mizani hii utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito", amesema Katibu Mkuu Nyamhanga.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

Aidha, Eng. Nyamhanga amewaagiza mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti uharibifu wa barabara.

Amewataka  madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
Katibu Mkuu Nyamhanga ametoa wito kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao ili kukuza uchumi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Amemataka  mkandarasi wa sehemu ya barabara ya Mela - Bonga (km88.8)  kuhakikisha anakamilisha kazi zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CHICO anayejenga sehemu ya barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.

Katika hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Hivyo makala KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)

yaani makala yote KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/katibu-mkuu-nyamhanga-aagiza-ujenzi-wa_7.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KATIBU MKUU NYAMHANGA AAGIZA UJENZI WA MIZANI BARABARA YA DODOMA – BABATI (KM 263)"

Post a Comment