DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA

DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA
kiungo : DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA

soma pia


DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA

Na Raufa Mrope 
Mwambawahabari
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji na uondoaji wa majitaka jijini humo na katika baadhi ya miji ya mkoa wa Pwani.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Romanus Mwang’ingo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema miradi hiyo inalengo la kuongeza upatikanaji maji,kusambaza maji katika maeneo mbalimbali,kukusanya na kusafisha majitaka.

Amesema kuwa mahitaji ya maji kwa jiji la Dar es salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo ni mita za ujazo 544,000 kwa siku na uzalishaji wa maji kutoka katika vyanzo vya visima na mitambo ya Ruvu juu, Ruvu chini na mtoni ni mita za ujazo 502,000 kwa siku.

“maji yetu kwa sasa tunatoa kwenye mto Ruvu ambapo tunatoa asilimia 88 tuna mtambo mdogo mtoni ambao unatoa asilimia 3na asilimia zilizobaki tunatoa kwenye visima ambavyo tumechimba maeneo mbalimbali ya jiji”,alisema.

Aidha Mwang’ingo ametaja miradi ambayo imekamilika na kupelekea ongezeko la maji jijini humo kuwa ni mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu chini na Ruvu juu, mradi wa uboreshaji mfumo wa usambazaji maji,miradi ya ukusanyaji na uondoaji wa majitaka na mradi wa uchimbaji wa visima Halmashauri mpya ya Ubungo.

Mbali na utekelezaji wa miradi hiyo DAWASA wanaendelea na utekelezaji wamiradi mingine katika miji mitano iliyo karibu na Dar es salaam ambayo ni Kibaha, Bagamoyo, Mkuranga,Kisarawe na Kilindoni-Mafia.

“sasa hivi tunafanya usanifu wa mfumo wa majitaka na majisafi katika mji wa Kibaha na Bagamoyo na miradi ya kuongeza maji katika miji ya Mkuranga, Kisarawe na Kilindoni-Mafia tayari tumekamilisha miradi Kibiti na ikwiriri”,alisema.

Hata hivyo ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo ni upatikanaji wa fedha, uhaba wa maeneo kwa ajili ya kuwekeza miundombinu, ongezeko la watu na kasi ya ukuaji wa mji ambao hauendani na kasi ya utekelezaji.

Mwang’ingo ameongeza kuwa ilikukamilisha miradi hiyo wanahitaji tirioni 2.8 na kwasasa wana tirioni 1.1hivyo wanashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha wanapata fedha hizo na kutekeleza azma yao.

Ifahamike kuwa DAWASA ni Shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1997 likiwa na jukumu la kutoa huduma ya Majisafi pamoja na Majitaka ,kabla ya hapo Majitaka yalikuwa chini ya Halmashauri ya jiji.


Hivyo makala DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA

yaani makala yote DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/dawasa-yaongeza-uzalishaji-wa-maji-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DAWASA YAONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KWA AJILI YA VIWANDA"

Post a Comment