title : TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA
kiungo : TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA
TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza (TAKUKURU) imethibitisha kuwahoji wanafamilia wa soka wakiwemo Mjumbe Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA) Shaffih Dauda na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Almas Kasongo.
Mbali na hao TAKUKURU wamethibitisha pia kuwahoji Elias Mwanjali, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo, Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa , Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola na wajumbe wa mikoa ya jirani kwasababu ya kuwepo kwa viashiria vya rushwa na kampeni.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale amethibitisha kuwahoji kwa wanafamilia hao wa mpira ambapo waliwashikilia tokea jana saa 3 usiku na wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na watakapojiridhisha wanaweza kuwakamata tena.
Taarifa inasema kuwa wanafamilia hao walitumia mgongo wa Ndondo Cup kufanya jambo lao usiku wa saa 3 jana na ndipo walipotiliwa shaka na kufuatiliwa na kutiwa mikononi mwa Takukuru ambao wamethibitisha kuwashikilia tokea jana usiku na kuwaachia kwa dhamana
Hivyo makala TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA
yaani makala yote TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/takukuru-mwanza-yathibitisha-kuwahoji.html
0 Response to "TAKUKURU MWANZA YATHIBITISHA KUWAHOJI WANAFAMILIA WA SOKA NA KUWAACHILIA KWA DHAMANA"
Post a Comment