title : SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
kiungo : SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali imewataka viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania pamoja na watetezi wa haki za wafugaji kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima, ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara Nchini hali ambayo imekuwa ikirUdisha maendeleo nyuma
Akizungumza jijini hapa katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii
“Serikali tunaomba sana watetetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Raisi Magufuli katika sera ya viwanda”Alisema Mwakiposa
Aidha alisema kuwa sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri watanzania walio wengi zaidia asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera ya viwanda hapa nchini
Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa akizungumza leo katika warsha ya siku tatu jijini Arusha iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini , mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo watetezi hao ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha).
Hivyo makala SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
yaani makala yote SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/serikali-yawataka-viongozi-wa-chama-cha.html
0 Response to "SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI"
Post a Comment