SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA
kiungo : SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA

soma pia


SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao hawajasajili, kujisajili katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri Mhagama alitoa agizo hilo jijini Mbeya Julai 27, 2017 wakati wa zoezi la ukaguzi wa kushtukiza jijini humo kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka waajiri wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara kujisajili kwenye Mfuko huo.

“Mwajiri ambaye hajajisajili kwenye Mfuko, anaweza kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi cha fedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5 jela au vyote kwa pamoja, hivyo nawasihi waajiri kutoka sekta binafsi na umma Tanzania Bara ambao hawajasajili kutekeleza sheria hiyo inayowataka kujisajili WCF katika muda huo nilioutoa.” Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.

Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mhe. Waziri alifuatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge na Afisa Kazi wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya ambapo taasisi ya kwanza ambayo Mhe. Mhagama aliikagua ni Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na St. Aggrey iliyoko Uyole na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika Mfuko.

Aidha Waziri alitoa siku saba kwa waajiri wote Mkoani Mbeya wapatao 107 ambao bado hawajajisajili ikiwemo Hospitali ya K’s na Shule ya sekondari St. Aggrey kujisajili ndani ya muda huo.

“Mkishindwa kutekeleza agizo hilo maana yake mnatuelekeza kutumia kifungu cha 71(4), cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kinachotamka adhabu ya faini ya kiasi cha fedha kisichopungua shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja.” Alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza leo Julai 27, 2017 wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa kushtukiza kwenye Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati jijini Mbeya ili kubaini kama mwajiri kwenye hospitali hiyo amejisajili katika  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). Waziri ametoa siku 30 kwa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, kujisajili na Mfuko huo, vinginevyo watakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo faini ya shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdusalaam Omar.

 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya, (kulia), wakiuliza alipo mkurugenzi wa Hospitali ya K's mara baada ya kuwasili na waziri Mhagama katika ziara ya ukaguzi wa kushtukiza leo Julai 27, 2017.
 Waziri Mhagama, (wakwanza kulia), Bi. Laura na Dkt. Omar, wakimsubiri Mfanyakazi huyu wa K's Hospital akiwasiliana kwa simu na mwajiri wake ili kumjulisha uwepo wa Waziri na ujumbe wake kwenye hospitali hiyo.
 Maafisa wa polisi wakiwa tayari kuhakikisha usalama unazingatiwa wakati wa zoezi hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA

yaani makala yote SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/serikali-yatoa-siku-30-kwa-waajiri-kote.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA"

Post a Comment