title : Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje
kiungo : Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje
Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje
Na: Lilian Lundo
Hayo yamesemwa leo, Jijini Dar es Salaam na mfanyabiashara wa korosho kutoka Mtwara Bi. Sakina Ponella katika uwanja wa Mwalimu Nyerere, yanapofanyika maonesho hayo.
"Kutokana na ubora wa korosho ninazouza, nimefanikiwa kupata wateja kutoka nchi za Uturuki, China, Syria na Rwanda," amesema Sakina.
Amesema kuwa mmoja wa wateja hao waliotembelea banda lake, amehitaji kutumiwa tani 4000 za korosho kila mwezi. Lakini kutokana na zao lenyewe kuwa la msimu, hivyo amemuelisha mteja huyo awe anatumiwa tani nyingi zaidi kipindi cha msimu wa zao hilo badala ya kutumiwa kila mwezi.
Sakina ameongeza kuwa, tayari wamebadilishana namba za simu na wateja hao kwa ajili ya hatua ya kuandikishiana mikataba na kuanza kutuma korosho hizo.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa kampuni ya Moringa (Mlonge) Natural Product kutoka Arusha, Leah Moses amesema maonesho hayo yamewasaidia kujulikana zaidi nje na ndani yaTanzania.
Amesema kuwa wamefanikiwa kupata wateja kutoka nchi za Kongo, Nairobi na China, ambao pia wamechukua namba za mawasiliano ya kampuni hiyo kwa ajili ya kuagiza bidhaa nyingine zaidi.
Aidha, mfanyabiashara wa vinyago kutoka Mtwara, Bi. Salma Omary amewata wafanyabiashara wadogo wadogo kutumia fursa ya maonesho mbalimbali ya biashara kujitangaza ili kupata masoko ndani na nje ya nchi.
"Wafanyabiashara hawatakiwi kufikiria juu ya kupata faida peke yake katika maonesho kama haya. Lakini wanaweza kutumia fursa ya maonesho ya biashara kwa ajili ya kujitanga zaidi ambapo itawaletea wafanyabiashara wengi zaidi wa kudumu,' amesema Bi. Salma.
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yalifunguliwa rasmi Julai 1 mwaka huu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Maonesho hayo yalitarajiwa kufungwa Julai 8 mwaka huu. Aidha Rais Magufuli alitoa agizo la kuongezwa siku 5 zaidi ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kujitangaza, vile vile kwa Watanzania kujifunza juu ya uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa.
Hivyo makala Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje
yaani makala yote Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/maonesho-ya-sabasaba-yatoa-fursa-ya.html
0 Response to "Maonesho ya Sabasaba Yatoa Fursa ya Masoko ya Nje"
Post a Comment