title : DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO
kiungo : DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO
DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO
Na Mathias Canal, WK-Simiyu
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ametangaza kuwa maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yatafanyika Mkoani Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2018 mpaka 2020 ili kuongeza tija ya elimu kuhusu sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa wananchi wa kanda ya Ziwa Mashariki.
Waziri wa kilimo Mhe Tizeba ametanga neema hiyo kwa wananchi wa kanda ya ziwa Mashariki jana tarehe 8 Agosti 2018 kwa wakazi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara ambayo inaunda kanda ya ziwa Mashariki ambao watanufaika na elimu kuhusu kilimo, mifugo na uvuvi.
Alisema kuwa kumekuwa na utaratibu wa kufanyika mfululizo maonesho hayo kwenuye mikoa inayoandaa huku akieleza kuwa utashi uliopo katika kanda hiyo ni mkubwa ukilinganisha na maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwa miaka minne mfululizo katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Alisema kuwa kufanyika mfululizo kwa miaka mitatu mkoani Simiyu kutawafanya wananchi kuwa na uhakika wa bidhaa za uwekezaji watakazoziweka. “Mkoa wa Simiyu na kanda yenu hii ya Magharibi ingetosha kuonyesha hata kwa miaka miwili tu lakini nimeamua kutumia utaratibu mzuri zaidi ili ifanyike kwa miaka mitatu naamini hamtaniangusha” Alikaririwa Mhe Dkt Tizeba
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akipongeza juhudi zilizofanywa na serikali na wadau wa kilimo katiika kufanikisha maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu wakati akitoa taarifa ya maonesho ya Nanenane mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benjamin Mkapa, Jana Tarehe 8 Agosti 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally wakati wa kilele cha maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018.Baadhi ya mamia ya wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga wakifatilia akwa makinbi maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yaliyofanyika kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Jana Tarehe 8 Agosti 2018.
Hivyo makala DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO
yaani makala yote DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dkt-tizeba-atangaza-maonesho-ya.html
0 Response to "DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO"
Post a Comment