title : JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
kiungo : JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka watumishi wa halmashauri ya mji wa Tarime na Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hizo mbili wakati wa ziara yake leo wilayani Tarime mkoani Mara.
Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kutembelea miradi ya afya, elimu, daraja na ujenzi wa nyumba za watumishi.
Jafo ameiagiza viongozi wa halmashauri hizo mbili kukaa na kufanya maamuzi ya majengo ya halmashauri ya wilaya ya Tarime yaliyopo ndani ya eneo la halmashauri ya mji yatumike kwa matumizi ya kiofisi ya halmashauri ya mji.
Aidha ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri ya mji zihamishiwe halmashauri ya wilaya ili waende kuanza ujenzi wa ofisini katika eneo lao badala ya kukaa ndani ya eneo la halmashauri mji.
“Kitendo hichi kinawakosesha wananchi haki yao ya kupata huduma kwa ukaribu jambo ambalo ndilo lilikuwa msingi wa kugawa halmashauri hizo,”amesema Jafo
Naibu Waziri Jafo amemaliza ziara yake na kuelekea wilaya ya Rorya, mkoani Mara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea eneo la mapokezi la hospitali ya Tarime na kuagiza lijengwe banda kwa ajili ya kukaa wananchi badala ya kukaa juani kama ilivyo hivi sasa. 
Watumishi wa Halmashauri mbili za Tarime wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Majengo yaliyojengwa na wadau wa mgodi wa North Mara kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Watumishi wa Halmashauri mbili za Tarime wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Majengo yaliyojengwa na wadau wa mgodi wa North Mara kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Hivyo makala JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
yaani makala yote JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/jafoacheni-kufanya-kazi-kwa-mazoea.html
0 Response to "JAFO:ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA"
Post a Comment