title : TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI
kiungo : TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI
TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI
Tanga: Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), imejiwekea malengo zaidi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 122 katika mwaka huu mpya wa fedha 2018/19 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki ili waweze kuchangia mfuko mkuu wa fedha za serikali.
Akifunga mafunzo ya siku nne ya kuhusu taratibu za kukusanya maduhuli ya serikali iliyofanyika katika ukumbi wa VETA mjini hapa, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo hilo litatilia mkazo uibuaji vyanzo vipya vya mapato.
“Nawashukuru watumishi wote wa TFS kila mmoja kwa nafasi yake, uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mhe Waziri Dkt. Hamisi Kigwangala, Bodi ya Ushauri iliyomaliza muda wake chini ya mama Ester Mkwizu na wajumbe wote kwa uchapakazi na uongozi thabiti uliowezesha TFS kukusanya na hatimaye kuwasilisha sehemu ya mapato yake kwa serikali.
“Kwa kweli ni fahari kwetu kama taasisi kuweza kuwasilisha bilioni 22.41 katika mfuko huo wa serikali kiasi kwamba tumeshika nafasi ya tano katika utoaji wa gawiwo hilo,” amesema Profesa Silayo.
Akizungumzia mikakati ya TFS katika mwaka huu wa fedha, Profesa Silayo amewataka watendaji wake kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato visivyokuwa na madhara katika shughuli za uhifadhi ili kuondoa dhana iliyojengeka kwamba vya taasisi hiyo kazi yao ni kuuza mbao na mkaa.Kusoma zaidi BOFYA HAPA>>>>>>>>>
Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
Picha ya Pamoja Mtendaji Mkuu wa TFS akiwa na wahasibu wa TFS Tanzania nzima mara baada ya kufunga mafunzo yao katika Ukumbi wa Veta jijini Tanga Ijumaa jioni.
Hivyo makala TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI
yaani makala yote TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tfs-yaja-na-malengo-ya-kuchangia-zaidi.html
0 Response to "TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI"
Post a Comment