title : HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA
kiungo : HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA
HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA
SERIKALI imemsomea Mashtaka saba Mwenyekiti wa Quality Group Yusuf Manji na wenzake watatu yakiwamo ya Uhujumu uchumi na usalama wa nchi
Kesi walisomewa Kwenye Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipolazwa Mtuhumiwa namba moja Yusuph Manji Mbele ya Hakimu Mkazib wa mahakama ya Kisutu Huruma Shahidi Wakili wa Serikali Kishenyi Mitalemwa aliwaomea washtakiwa mashataka yao.
Watuhumiwa wengine ni Pamoja na Abdala Sangey, Deogratias Kisimba, na Tobias Fwele
Shtaka la Kwanza Tarehe 30 Juni 2017 eneo la Changombe Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na Askari Polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa yanayotumika kutengenea Sare za Polisi zenye Thamani ya Milioni 192.5
Shtaka la Pili watuhumiwa wote Tarehe 30 Juni walikutwa na Mabando Manane ya vitaambaa zinazotumika kutengeneza JWTZ.
Kosa la Tatu watuhumiwa walikuwa kukutwa na mihuri ya serikali washtakiwa wote kwa pamoja tarehe 1 July walikutwa na mihuri ya jeshi la Tanzania iliyoandikwa "Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha jeshi JWTZ "bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi.
Kosa la Nne watuhumiwa walikutwa na Mhuri wa Serikali walikutwa na muhuri wa JWTZ yenye maandishi Kamanda kikosi 834 KJ makutupola Dodoma bila kuwa na uhalali kitendo
Shtaka la tano kukutwa na Mhuri wa Serikali wenye maneno "COMMANDING Oficcer 835 kj Mgambo P.O.BOX..."
Shtaka la sita kukutwa na mali inayozaniwa kupatikana isivyo halali Tarehe 1 Julai Changombe Plate namba SU 383 ambayo ilipatakana isivyo halali.
Washtakiwa Hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu wanashtakiwa kwa sheria ya Uhujumu Uchumi na usalama wa taifa.
Hakimu Shahidi amesema Kwamba masuala hayo yasikilizwe kwenye Mahakama yenye mamlaka.
kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 19 mwezi Julai upelelezi wa Kesi haujakamilika.
Mbali na hilo gazeti hili lilijaribu kumtafuta wakili wa washtakiwa, Hudson Ndusyepo ili atoe ufafanuzi juu ya kile kinachowakabili Wateja wake lakini mpaka tunaondoka katika viwanja vya hospitali ya Muhimbili hatukufanikiwa kuwapata.
Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita mawakili wanaomtetea Manji waliiomba mahakama kuu kuingilia kati suala la Mteja wao kutokana na kukamatwa pamoja na kushikiliwa isivyo halali.
Mawakili hao waliweza kuwasilisha maombi kwa hati ya dharura wakiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuwataka walalamikiwa wafikishwe mahakamani ili washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Hivyo makala HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA
yaani makala yote HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/haya-hapa-mashtaka-aliyosomewa-yusuf.html
0 Response to "HAYA HAPA MASHTAKA ALIYOSOMEWA YUSUF MANJI KITANDANI MUHIMBILI ALIPOLAZWA"
Post a Comment