Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko

Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko
kiungo : Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko

soma pia


Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko


MJASIRIAMALI mdogo wa Mlandizi, mkoani Pwani, Elisiana Laizer, leo ametangazwa kuwa mshindi wa droo ya 19 ya kuwania Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutikisa hapa nchini.

Droo ya kumpata mwanadada huyo ilichezeshwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehus Ngolo.

Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba ni furaha yake kuona droo tatu kati ya 19 zilizoendeshwa na Biko zimewapata wanawake watatu, jambo linaloonyesha kwamba mchezo wao umekuwa wa Watanzania wote.

“Ni jambo la kutia moyo kuona droo ya 19 imempata dada wa Mlandizi, Elisiana ambaye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo maeneo ya Mlandizi, mkoani Pwani, nikiamini kuwa ni hatua nzuri kwake na Kwa Watanzania wote wanaocheza Biko,” Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Biko imezidi kukolea baada ya kutoka Dodoma, ikaenda Mbeya sasa imetua mkoani Pwani kwa mshindi wao Elisiana ambaye ameibuka kidedea kwa Sh Milioni 20, huku zawadi mbalimbali za Biko za hapo kwa hapo zikianzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Tumetoka Mbeya juzi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wetu Linda Mhewa Sh Milioni 20 zake, huku leo tukimpata msichana mwingine anayeishi Mlandizi, mkoani Pwani aliyecheza Biko mchezo rahisi unaochezwa kwa ujumbe wa simu za mikononi wa Tigo Pesa, M-pesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema Biko ni mchezo rahisi wa ujumbe mfupi wa maandishi unaotoa ushindi kwa Watanzania wote, hivyo Watanzania wachangamkie fursa.

“Biko ni mchezo unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote, hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi ili wavune mamilioni ya zawadi kutoka kwenye mchez huu,” Alisema.
Hadi sasa tayari zimeshafanyika droo 19 za kutoa ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20, huku Biko wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa Mwezi Mei pekee tangu mchezo huo wa kubahatisha ulipoasisiwa nchini Tanzania na kutoa fursa ya utajiri kwa Watanzania.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, kushoto akizungumza jambo na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja katika kuchezesha droo ya 19 ya Biko ambapo mjasiriamali Elisiana Laizer kutoka Mlandizi, mkoani Pwani alifanikiwa kuwa mshindi wa Sh Milioni 20.



Hivyo makala Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko

yaani makala yote Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/elisiana-laizer-wa-mlandizi-mkoani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko"

Post a Comment