DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR

DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR
kiungo : DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR

soma pia


DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR

Na Is-haka Omar, Zanzibar.  
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia  jana (juzi) baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.   
Marehemu hao waliotambuliwa kwa majina ya Mwatma Mohamed Malawi (2), Haisam Mustafa(2), Munawar Ahmed Khamis (3) na Muslim Hamza bakar (2) wote wamezikwa leo katika maeneo tofauti ya Makaburi ya Mwanakwere na Kiembe samaki Mbuyu Mnene Unguja. 
Akizungumza mara baada ya maziko hayo Naibu Katibu huyo huko katika makaburi ya Mwanakwerekwe, alisema CCM imepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya vifo vya watoto hao na inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizopata msiba huo na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba huo.
Alisema watoto hao walitarajiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae hivyo msiba huo umeacha pengo kubwa  kwa familia na taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt. Mabodi aliwataka wazazi na walezi nchini kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha mazingira yanayotumiwa na watoto kucheza yanakuwa katika hali ya usalama ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha majeraha ama vifo kwa watoto wao.
 Maiti za watoto wanne waliofariki ndani ya gari huko Kidongochekundu  Zanzibar wakitolewa msikitini na kupelekwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya mazishi.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao. 


Hivyo makala DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR

yaani makala yote DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/dktmabodi-ashiriki-mazishi-ya-watoto.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT.MABODI ASHIRIKI MAZISHI YA WATOTO WANNE WALIOFARIKI NDANI YA GARI ZANZIBAR"

Post a Comment