Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake
kiungo : Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

soma pia


Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.

Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki. 

Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.

Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo. 

“Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh. Ngupula.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.



Hivyo makala Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

yaani makala yote Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/dkt-kigwangalla-akabidhi-gari-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake"

Post a Comment