BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI
kiungo : BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

soma pia


BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

Na Othman Khamis Ame
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Chama cha Skauti Nchini kuongeza nguvu za kuwaelimisha Vijana wenzao hasa walioko Vijijini ili wajikomboe kupenda kujishughulisha na kazi au miradi ya ujasiri amali.
Alisema Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na vigenge vya kihuni mitaani vinavyopelekea kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya wizi pamoja na vitendo vya kudhalilisha watoto wanawake na watu wenye mahitaji Maalum.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Mkoani Dodoma kushiriki Tamasha la Wiki Moja la Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania hapo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Alisema zipo fursa nyingi za ajira zinazopatikana katika Sekta ya Utalii ambazo Vijana endapo wataamua kuzichangamkia zinaweza zikawapatia kipato kwa kutumia soko la bidhaa zinazotokana na kilimo cha mboga mboga na mazao ya Baharini.
Balozi alifahamisha kwamba Uskauti kwa vile hauna mafungamano ya itikadi ya Kisiasa wala Dini unalengo la kuwaunganisha Vijana katika harakati zao za kimaisha kupitia misingi ya kujenga Utaifa wao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa vijana wa Skauti kufundishwa mbinu na mafunzo ya kuogelea na kuzamia kutokana na majukumu yao yaliyowazuunguka ya kuwa wao ni miongoni mwa Taasisi zinazotoa huduma wakati yanapotokea maafa au majanga.
Balozi Seif alielezea kuridhika kwake na Kanuni 10 za Skauti zinazoelekeza uzalendo unaojenga Taifa lenye Wananchi wanaopendana na kuwa na nguvu za kukabiliana na changamoto zinazowazunguuka katika misingi ya nidhamu na uwajibikaji.
Mapema Kamishna Mkuu Msaidizi wa Chama cha Skauti Zanzibar Maalim Suleiman Takadir alisema Skauti iliasisiwa Zanzibar mnamo mwaka 1912 na Mwaka 1917 ikaanzishwa upande wa Tanzania na kufifia katika miaka ya 60.
Maalim Takadir alisema Chama hicho kilianzishwa tena Mwaka 1992 chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour ili kufufua ari ya kuwajenga Vijana katika uzalendo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akivishwa Skafu na Kijana Omar Amour Said wa Skauti nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar kabla ya kuzungumza na Vijana wa Chama cha Sakauti Zanzibar. Kati kati yao ni Raius wa Chama cha Skauti Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma.
Balozi Seif akiambatana na Rais wa Skauti Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma wakielekea ndani ya Ukumbi wa Mkutano kuzungumza na Vijana wa Skautio Zanzibar wanaotarajiwa kuondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Dodoma katika maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania.

Balozi Seif akimpongeza Kijana Kassim Yussuf Msoma Mashairi ghibu baada ya kughani kwenye Mkutano wa Skauti Zanzibar uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
Baadhi ya Skauti wa Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Chama hicho uliohutubiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uliokuwa wa matayarisho ya mwisho wa Vijana wake kujiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.
Baadhi ya Makatibu wa Skauti wa Mikoa ya Unguja wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif ambaye hayuko pichani hapo katika Ukumbi wa zamia wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwahutubia VBijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.Picha na – OMPR – ZNZ.


Hivyo makala BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

yaani makala yote BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/balozi-seif-akitaka-chama-cha-skauti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI"

Post a Comment