title : Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band
kiungo : Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band
Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band
Baada ya kauli ya Beka Flavour kuwa hatomvumilia Aslay iwapo atatoa ngoma nyingine, Aslay amesema hilo halina shida.
Aslay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Baby’, amesema hafikirii kuwa kitendo cha Beka Flavour kuhairisha kutoa ngoma ili zisigongane na yake ni kumuhofia kwani ni msanii mzuri mwenye muziki mzuri.
“Mfano mdogo Libebe imepita na hata angeamua kutoa ngoma na mimi zingekutana huku mjini na kila shabiki angependa ngoma kwa wakati wake,” Aslay ameiambia E-Newz ya EATV.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa kitendo cha Beka kuhairisha kutoa ngoma kinaweza kuwa sawa lakini angependa kumuona akitoa kazi nyingi zaidi kwa kuwa ni ndugu yake.
Alipoulizwa kuhusu kauli ya Beka kuwa yeye ni mdogo kwake kimuziki alijibu, “mimi ni mdogo kweli, hivyo tu”.
By Peter Akaro
Hivyo makala Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band
yaani makala yote Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/aslay-akubali-yaishe-kwa-beka-wa-yamoto.html
0 Response to "Aslay akubali yaishe kwa Beka wa Yamoto Band"
Post a Comment