title : YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI
kiungo : YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI
YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga imekuwa timu ya kwanza toka Tanzania kutinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penati.
Katika mchezo wa kwanza Singida United ilicheza dhidi ya AFC Leorpads ya Kenya na vijana hao wa Hans Van Der Pluijm walitolewa kwa penalti 5-4
Yanga imeing’oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.
Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung’olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao.
Yanga sasa watakutana na AFC Leorpads siku ya Alhamis na Fainali ya Michuano hiyo itachezwa siku ya Jumapili Juni 11 na bingwa atacheza na Everton katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam July 13 mwaka huu.
Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) akichuana na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga Chipukizi na Tusker ya Kenya wakichuana katika mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Picha zote na Montage Ltd
Hivyo makala YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI
yaani makala yote YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/yanga-yatinga-nusu-fainali-ya-sportpesa.html
0 Response to "YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI"
Post a Comment