title : WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO
kiungo : WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO
WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Katika hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia shilinginTrilioni 1.3.
Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira." Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu mbalimbali za ujasiriamali.
Kuhusu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa vijana.
"Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji." Alisema Bw. Mayingu. Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza.
Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo, Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
Washiriki wakijadiliana.
Hivyo makala WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO
yaani makala yote WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/wastaafu-pspf-mwaka-201718-kulamba.html
0 Response to "WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO"
Post a Comment