WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI
kiungo : WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

soma pia


WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

Na Ramadhani Ali – Maelezao Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameshtushwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na homa ya Ini wakati wananchi wengi hawana uelewa juu ya maradhi hayo na Serikali haijaandaa mikakati imara ya kupambana nayo.

Wajumbe hao walieleza hisia zao wakati wakichangia mada ya hali halisi ya homa ya Ini katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu maradhi ya Kifua kikuu, Ukimwi na Homa ya Ini ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi alisema wakati homa ya Ini inaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi ikilinganisha na maradhi mengine haikuzungmzwa katika Bajeti ya mwaka huu ya Wizara ya Afya.

Amesema kukosekana taarifa ya homa Ini ndani ya Bajeti ya Wizara huku wananchi hawana uelewa juu ya homa hiyo itapelekea kuenea kwa kasi na kupoteza maisha ya wananchi.

Mwakilishi wa kuteuliwa Ahmada Yahya ameishauri Wizara ya Afya kupitia Kitengo Shirikishi kutoa taaluma zaidi kwa wananchi ili kuwa na uelewa mpana wa homa ya Ini na njia za kujikinga nayo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo ameishauri Kamati ya Bajeti ya Baraza hilo kuangalia uwezekano wa kukipatia fedha Kitengo Shirikishi cha Ukimwi, Kifua Kikuu na homa ya Ini ili kiweze  kukabiliana nayo.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo akiufungua rasmi katika Hoteli ya Ocean View (kulia) Mnadhimu wa Baraza  Ali Salim Haji na (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa kuwashahishaji kuhusu Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

yaani makala yote WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/wajumbe-wa-baraza-laawakilishi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI"

Post a Comment