title : SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020.
kiungo : SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020.
SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020.
NA WAMJW DAR ES SALAAM
SERIKALI imejidhatiti kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili kutimiza malengo ya kujenga uchumi wa viwanda na afya bora mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka unaolenga kupitia shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
“Tunataka mpaka kufikia 2020 tuwe tumetokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kama mabusha na matende ili kuweza kuinusuru nchi katika aina hii ya magonjwa yanayojitokeza katika nchi zinazoendelea hususan Tanzania” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa licha ya kudhibiti mabusha na matende pia wamejidhatiti kuzuia ugonjwa wa usubi na kichocho kabla ya kufikia 2025 ili kuendana na mpango wa dunia wa kudhibiti magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Taifa Wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kupata dawa na tiba za magonjwa hayo kwan hazina madhara kwa binadamu.
Mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka duniani kote umelenga kupata mpango kazi wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka 2017 na 2018 ili kuweza kupata njia za kudhibiti magonjwa hayo kama vile mabusha na matende, kichocho na usubi.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi akiwasirisha mchango wake mbele ya wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (Hawako kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa wa udhibiti wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akifuatilia kwa ukaribu mjadala uliokuwa ukiwasilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar kambi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, anaefuatia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe na mkurugenzi wa kinga Dkt Neema Ruzibamayila.
Wadau kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia mjadala kwa ukaribu katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele uliofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi (Hayupo kwenye Picha) uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.
Wadau wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wakiwa kwenye picha ya pamoja ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.
Hivyo makala SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020.
yaani makala yote SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/serikali-yajidhatiti-kutokomeza.html
0 Response to "SERIKALI YAJIDHATITI KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE KUFIKIA 2020."
Post a Comment