title : CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA.
kiungo : CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA.
CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA.
Mwambawahabari
Na Maria Kaira, mwambawahabari
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es salaam Saddy Kusilawe amemuomba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli kuwachukulia hatua viongozi wote walioshiriki kuhujumu rasilimali za nchi kwa kusafirisha makontena ya mchanga wa dhahabu ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao.
Kauli hiyo imetolewa leo kwenye kikao cha chama cha wilaya ya ubungo cha kumpongeza Rais Magufuli kwa shughuli anazofanya za kujenga nchi pamoja na kuwapigani wanyonge ikiwa ni lengo la kutekeleza ilani ya chama hicho.
"Lazima tuseme basi kwa kilichotokea na tulaani kitendo hiki, cha mafisadi wanaoshirikiana na watu wanaotoka nje ya nchi kuuza madini kinyemela bila kwa kuangalia masilahi ya nchi" alisema Kusilawe
Pia amesema anamuomba Rais Magufuli kuwachukulia maamuzi magumu ya kisheria viongozi wote walioshiriki kuhujumu rasilimali za watanzania za kusafirisha makontena ya mchanga wa dhahabu ili waweze kutambua kitu walichokifanya akiendani na taifa pamoja na watanzania kwa ujumla.
"Naraani kitendo kinachofanywa na baadhi ya watanzania wanaopinga hatua iliyochukuliwa na rais,hili nijambo zuri na watanzania tuungane kumuunga mkono rais kwa hatua aliyoichukua ya kupambana dhidi ya watanzania , watanzania tunatakiwa kitu kimoja tusiposhikamana kwenye vita hii tutashindwa kutekeleza maendeleo ya taifa" alisema
Kwa upande wa katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Salumu Abdalla amesema anamuomba rais Magufuli kuhakikisha anawachukulia hatua za kisheria na zakinizamu viongozi wote waliohusika kuhujumu rasilimali za watanzania kwa kuwaondoa katika nafasi zao pamoja na kutaifishwa mali zao.
"Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi ma milioni ya fedha yameenda nje bila utaratibu huku watanzania wanyonge wakibaki wanataabika bila sababu yoyote lazima tumuunge mkono mhe. Rais kwa hatua aliyochukua ni nzuri, wanachama wa wilaya ya ubungo sisis tunamuunga mkono rais" alisema
Aidha ametoa rai kwa rais John Magufuli kuendelea na kasi aliyoanza nayo ya kulitetea taifa ili kuweza kuwatetea wanyonge ikiwa na lengo la kutekeleza ilani ya chama hicho.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM kata ya Ubungo Alhaj Marussu amesema anakiomba chama hicho kuwafukuza uwanachama viongozi wote wanaotuhumiwa kuhujumu rasilimali za watanzania ili waweze kuhojiwa vizuri.
"Chama chetu kinaitaji viongozi walio wasafi wanaokuwa na uchungu na watanzania wenzao, lazima sheria ichukue mkondo wake kwa watuhumiwa hao" alisema
Pia amewaom ba wanasheria kukaaa kwa pamoja na kujadili nini kifanyeke juu ya jambo hilo.
Hivyo makala CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA.
yaani makala yote CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/ccm-wilaya-ya-ubungo-inamuomba-rais.html
0 Response to "CCM WILAYA YA UBUNGO INAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWACHUKULIA HATUA VIONGOZI WALIOHUJUMU RASILIMALI ZA TAIFA."
Post a Comment