MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA
kiungo : MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA

soma pia


MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda na kuhifadhi mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa huo Amos Makalla kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji katika wilaya za Mbarari na Chunya - Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa ushirikiano na watendaji wengine katika kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo yao.

Amesema kabla ya hatua kuchukuliwa ni vizuri wananchi wakaelimishwa kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kabla ya kuondolewa kwenye maeneo waliyovamia ikiwemo maeneo ya vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa Mbeya kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa ikolojia katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala pamoja na kikosi kazi chake wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-apokea-taarifa-ya-kikosi_14.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI KUTOKA MBEYA"

Post a Comment