title : RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
kiungo : RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Na Robert Hokororo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.
Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.
Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
Hivyo makala RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
yaani makala yote RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/rc-shinyanga-afanya-ziara-wilayani.html
0 Response to "RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO"
Post a Comment