Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar

Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar
kiungo : Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar

soma pia


Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar

Na Ali Issa –Maelezo Zanzibar.
Serikali imetoa fursa kwa vijana  kutengeneza sheria yao ili kuwawezesha kutekeleza shughuli zao katika Nyanja mbalimbali za kimaisha.

Hayo yamesemwa huko katika ukumbi wa wasanii Rahaleo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayuob Muhamed Mahmoud wakati akifungua mkutano wa dharura wa baraza la Vijana Taifa uliojadili kanuni, malengo na mpango mkakati wa baraza hilo.

Amesema mpango huo ni fursa pekee kwa vijana iwapo wataitumia vizuri hivyo amewataka kuwa makini wanapoijadili na kupitia vifungu vya kanuni na miongozo mengine ya baraza hilo.

Amewashauri wakati wa kuijadili taarifa hiyo kuhakikisha wanaingiza vipengele muhimu ambavyo wanahitajiwa kutekelezewa na Serikali.

“Jengeni mipango iliyobora kwa ajili yenu vijana na Serikali ipo tayari kuhakikisha mipango hiyo inatekelezwa,”alisema Ayuob.

Aidha aliwataka vijana wawe mstari wa mbele kwa kufanya kazi kwa kujitolea pamoja na kuthamini juhudi za viongozi na uhuru wa taifa lao

Mkuu huyo wa Mkoa aliishauri Wizara ya Kazi,Uwezeshaji Wananchi ,Vijana Wanawake na Watoto kulifungua Baraza hilo rasmi kutambulika kisheria kwani linajumuisha vijana wote wa Zanzibar kupitia ngazi za shehia, wilaya na mikoa.

Nae katibu Mtendaji wa Baraza hilo Khamis Faraji Abdalla alisema lengo la mkutano huo ni kupitia vifungu vya kanuni, mpango mkakati na vipengele vyengine vya kumuelekeza kijana umuhimu wake kitaifa katika harakati zake za kila siku.

Hata hivyo alisema mpango huo unavipengele vingi vya utekelezaji kwa vijana na ameahidi wataipitia ikiwa ni pamoja na kazi za kamati, nembo ya baraza,utaratibu wa nidhamu kwa vijana, mfumo wa mawasiliano kutoka ngazi ya shehia hadi taifa, dua na kiapo cha baraza.

Katibu huyo alimuhakikisha Mkuu wa wa Mkoa kwamba  watayafuata na kuyafanyia kazi maelekezo yake kama alivyoagiza.


Hivyo makala Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar

yaani makala yote Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mkutano-wa-baraza-la-vijana-zanzibar.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkutano wa Baraza la Vijana Zanzibar"

Post a Comment