title : Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko
kiungo : Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko
Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko
DROO ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imechezeshwa jana jana, huku ikimpata mshindi wake wa nonge nono la Sh Milioni 20 ikiwa ni maalum kwa Jumatano hiyo kutoa mshindi wa Sh Milioni 20 ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule kuibuka kidedea kwa kuzoa mamilioni hayo.
Donge nono hilo limekwenda kwa mshindi huyo wa Arusha, ikiwa ni mwendelezo wa kutoa mamilioni katika zawadi mbalimbali za bahati nasibu huyo inayoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja kwa zawadi za hapo hapo huku droo kubwa ya Jumatano na Jumapili hii pia itatoa Sh Milioni 20 kama Jumatano mbili zilizopita.
Akizungumza leo asubuhi katika uchezeshaji wa droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni wakati wa kushinda mamilioni ya Biko kwa kuchezesha bahati nasibu yao rahisi na yenye nafasi kubwa ya ushindi wa zawadi za papo kwa hapo na zile za wiki zinazotoa mamilioni kwa droo ya Jumatano na Jumapili.
Alisema hadi sasa zaidi ya washindi 55,000 wameshinda zawadi kutoka Biko, huku wakiamini kuwa Biko ni chanzo cha mapato na kinachoweza kubadilisha maisha ya washindi wao wanaoamua kujitokeza kwa wingi kuwania mamilioni kwa kupitia mchezo huo.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu kila mtu anaweza kucheza kwa kupitia simu yake ya mkononi hususan kwa Tigo, Vodacom na Airtel ambapo wataingia kwenye vipengele cha kufanya miamala kwenye simu hizo kwa kuingiza naamba ya kampuni ambayo ni 505050, huku namba yetu ya kambukumbu ikiwa ni 2456.
“Hakuna njia ya mkato ya kushinda Biko badala yake watu wanapaswa kucheza kwa wingi na mara nyingi zaidi ili wajiwekee nafasi nzuri za ushindi, ukizingatia kuwa ndio sababu kubwa ya ushindi maana kila anayecheza Biko jua anaweza kubadilisha maisha yake kama atashinda zawadi za papo hapo pamoja na ile droo kubwa ya Sh Milioni 10 hadi 20 kwa Jumatano hii na ile iliyopita pamoja na Jumapili inayokuja ambapo bado siku chache mshindi apatikane,” Alisema.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kushoto akiandika namba ya ushindi ya mkazi wa Arusha, Oscar Haule katika droo ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo.
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Arusha, Oscar Haule, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Hivyo makala Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko
yaani makala yote Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mkazi-wa-arusha-oscar-haule-aibuka-na.html
0 Response to "Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko"
Post a Comment