title : MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.
kiungo : MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.
MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.
Na Abdullatif Yunus, Kasibante Fm.
Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Ipo katika Mkakati na Hatua za Awali za kuyapeleka Makao Makuu ya Wilaya Bukoba, katika tarafa ya Rubale, Kata Rubale.
Hayo yamebainika katika Mkutano wa Hadhala wa Wananchi pamoja na wadau wa Elimu, uliofanyika katika Kata ya Rubale Juni 3, 2017.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze amesema, tayari Halmashauri imekwishatuma timu ya Wataalamu kukagua maeneo wapi panafaa kuwekwa Makao Makuu hayo ya Wilaya, Rubale ikiwa ni eneo mojawapo linalopewa kipaumbele, hivyo wananchi wawe tayari kuyapokea maamuzi hayo pale yatakapopitishwa.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Mwenyekiti Ngeze amesema kuwa tayari mazungumzo ya awali yameanza kufanyika ikiwa ni pamoja na kuanza mipango ya kuanza kuifanya Rubale kuwa Mji mdogo, huku akitoa Rai kwa Wananchi kukubali usumbufu na uharibifu utakaojitokeza kuhusiana na mali zao, kwani Maendeleo pia huambatana na hasara.
Awali mwenyekiti Ngeze ambae pia ni Diwani wa Kata ya Rukoma, amewapongeza wananchi kwa kujitolea kuchangia vifaa vya ujenzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Rubale, na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani mbalimbali ili kuchangia Ujenzi wa Shule hiyo, na kusisitiza kuwa Shule hiyo ambayo inapendekezwa kuwa ya Wasichana pekee ni lazima itajengwa Rubale.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Tarafa Rubale kupitia CCM, Bi Asuma Kokugonza Bantanuka amewaomba akina mama kujitokeza kwa wingi kuunga mkono Ujenzi huo, na kuwataka wnawake ikibidi kujitoa na kujitolea kufanikisha zoezi hilo, lengo likiwa ni kumsomesha mtoto wa kike kwa maendeleo ya Baadae.
Bi Asuma aliefuatana na Mwenyekiti Ngeze Katika ziara hiyo ameongeza kuwa, mwanamke ana nafasi na jukumu kubwa katika jamii hasa katika suala la maendeleo hivyo, hana budi kubaki nyuma ili kujikwamua kiuchumi.
Diwani viti maalum Tarafa Ruabale - CCM Bi Asuma Kokugonza Bantanuka akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo..
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Mhe. Murshidi Hashim Ngeze akizungumza na hadhara iliyohudhuria mkutano wake eneo la Katani, Rubale.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiendelea kufuatilia hotuba.
Picha zote na Allawi Kaboyo
Hivyo makala MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.
yaani makala yote MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/makao-makuu-ya-halmashauri-ya-wilaya.html
0 Response to "MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE."
Post a Comment