MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU

MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU
kiungo : MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU

soma pia


MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema jeshi la Polisi katika Mkoa huo linatakiwa  kuwa la mfano wa kuigwa katika kukabiliana na kila wimbi la uhalifu, ili wananchi waishi kwa amani kutokana na umuhimu wa biashara.

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa kupeleka magari  26 ya polisi  kwenye ukarabati katika gereji  iliyoko  maeneo ya Utalii mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya matengenzo pamoja na ufungaji wa Kamera katika magari  hayo alipokuwa anazungumza na jeshi la polisi leo  Osterbay  jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kukabiliana na rushwa na jeshi hilo, watafunga kamera katika kila kituo ndani ya jiji la Dar es Salaam,  ambapo OCD , kanda maalumu, pamoja  na Mkuu wa Jeshi la Polisi  wataweza kuona kile ambacho kinafanyika. 

Makonda amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam linatakiwa kuwa la kisasa zaidi katika kukabiliana na uhalifu wa kila namna ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa.

Amesema katika maboresho hayo wataweka Kompyuta kila kituo ili  kuachana na kuandika maelezo katika karatasi na mtu yeyote,  baada ya kuwekwa kompyuta hizo asikubali kuandikiwa maelezo katika karatasi.
Aidha amesema kuna baiskeli ziko njiani ambazo zitagawiwa kwa polisi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uhalifu katika mazingira ambayo kifaa hicho kinaweza kupita.

 Nae Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya  amesema Jeshi la Polisi kanda maalumu inakabiliwa na changamoto ya magari pamoja na mafuta na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi katika kukabiliana na wahalifu wa kila namna .

Amesema kuwa kutokana maboresho hayo yataweza kubadilisha hata takwimu zilizo katika kipindi hiki zisirudie kutokana na maboresho hayo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watendaji  mkoa  na polisi katika hafla ya upelekaji wa gari 26 ya jeshi la polisi katika matengenezo mkoani Kilimanjaro leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu magari yaliyoharibika  kwa ajili ya kwenda katika matengenezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  (kulia) na watatu kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Ally Hapi leo katika Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es Salaam.
 Moja ya gari mbovu ya Polisi ikiwa tayari kwa kusafirishwa kwa ajili matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wanajeshi wataopeleka magari kwa ajili ya matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika leo katika kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU

yaani makala yote MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/makonda-kubadili-jeshi-la-polisi-kwenda.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKONDA KUBADILI JESHI LA POLISI KWENDA KISASA KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU"

Post a Comment