MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO

MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO
kiungo : MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO

soma pia


MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO


Mabenki yameombwa kuwa tayari kukopesha mnyonyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Bw. Chacha amesema kuwa mabenki na taasisi za kifedha nchini hazina budi kuwekeza mtaji wa kutosha ili kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Tanzania na ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

Ameongeza kuwa kuanzinshwa kwa TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara kupata fedha zenye masharti nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta ya kilimo ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.
Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda (kulia) akizungumza nafasi ya TADB katika kuwezesha Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kuweza kukopesha wakulima.
Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya kufanyia uchambuzi miradi ya kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa mikopo kwenye sekta hiyo.



Hivyo makala MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO

yaani makala yote MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mabenki-yaaswa-kukopesha-sekta-ya-kilimo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MABENKI YAASWA KUKOPESHA SEKTA YA KILIMO"

Post a Comment