Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.

Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.
kiungo : Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.

soma pia


Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii .


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu alikamatwa baada kutolewa kwa amri ya kufanyika hivyo kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum (ZCO).  

MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu MKazi Godfrey Mwambapa wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu ilipokuja kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, Mgonja amedai kuwa Juni 28, mwaka jana, ZCO Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika Viwanja vya mahakama hiyo.

Amedai, Juni 29 mwaka jana, majira ya mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni ambapo alimkamata na kumfikisha katika Ofisi za ZCO na kumkabidhi.

Alidai kuwa, alipewa amri na ZCO kumkamata Lissu  na alifanya hivyo licha ya kuwa hakuwa na hati ya ukamataji kwa kuwa mamlaka yalikuwa yanamruhusu kufanya hivyo na kuwa mtu yoyote akifanya makosa ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati. 

Aliongeza kuwa, kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa, “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, “huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu”. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’


Hivyo makala Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.

yaani makala yote Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/kesi-ya-lugha-ya-uchochezi-dhidi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani."

Post a Comment