title : KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Dotto Mwaibale
JAMII imetakiwa kujenga moyo wa kusaidia watu waliopo katika makundi yenye uhitaji ili nao wajisikie kama watu wengine waliopo katika familia.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark inayojishughulisha na uwezeshaji jamii, Agnes Mgongo wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa zawadi ya Sikukuu ya Eid El-Fitr katika Kituo cha watoto Yatima cha Mtoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo hii.
"Ni vizuri jamii ikajenga tabia ya kuwakumbuka watoto na watu wengine waliopo katika makundi maalumu kwa kuwafariji badala ya kuiachia serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya" alisema Mgongo.
Alisema kampuni yake iliguswa na changamoto walizonazo watoto waishio katika kituo hicho ikaona ni vizuri katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El-Fitr wakajumuike nao kwa kula na kucheza pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.
Mgongo alitaja zawadi walizotoa kupitia wadau wengine marafiki wa taasisi hiyo kuwa ni nguo, vinywaji na chakula ambacho kilipikwa katika kituo hicho.
Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo watoto waliopo katika makundi yenye uhitaji, Wanswekula Zacharia alisema ni pamoja na vitabu, karo, sare za shule na mahitaji mengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa amekaa na watoto wa kituo hicho.
Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.
Hivyo makala KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/kampuni-ya-trumark-yatoa-zawadi-ya-eid_27.html
0 Response to "KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment