title : Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko
kiungo : Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko
Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko
DROO ya 13 ya Biko waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha Tanzania maarufu kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, imefanyika leo asubuhi, huku mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaa, Amani Kabuku, mwenye miaka 23, akifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh milioni 20.
Mshindi huyo ameibuka katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Akizungumza katika droo hiyo leo asubuhi, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kupitia mchezo wao wa Biko uliozidi kujizolea umaarufu katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.
Alisema anaamini washindi wao wanaoendelea kujipatia fedha mbalimbali kupitia mchezo wao, huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza kwa kufanya miamala ya fedha kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000, ambapo namna ya kucheza ni kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.
“Wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri yaushindi wa zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zikilipwa moja kwa moja kupitia simu zao za mikononi walizotumia kuchezea Biko,” Alisema Grace.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kulia akiwa kwenye majukumu ya kumtafuta mshindi wa droo ya 13 ya Biko ambapo kijana mwenye miaka 23 mkazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam, Amani Kabuku, alifanikiwa kuibuka na zawadi nono ya Sh Milioni 20. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Kajala Masanja kulia akizungumza huku akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko
yaani makala yote Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/amani-kabuku-wa-dar-es-salaam-aibuka.html
0 Response to "Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko"
Post a Comment