title : 30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili
kiungo : 30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili
30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili
MwambawahabariMkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (wa tatu kutoka kushoto) akipokea kifaa cha sterilizing kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida (kulia). Kutoka Kushosho ni Mkuu wa Idara ya Macho Muhimbili, Dk Mtemi Baruani na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Yamasaki Eye, Dk Takashi Yamasaki na Kenji Takeuchi wa Take Opht Medical Corporatio. Kifaa hicho kitatumika wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya macho.
Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimshukuru Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida baada ya kuupokea Leo
Mmoja wa wataalamu wa Afya kutoka Japan, Chika Yoshinda akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kifaa hicho, jinsi ya kikutumia na kukitunza.
Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na Serikali ya Japan wakimsikiliza, Chika Yoshinda.
…………………..
Timu ya Madaktari kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na MUHAS wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagojwa 30 wenye matatizo ya mtoto wa jicho.
Akipokea msaada wa kifaa cha utakasaji ( Sterilizing instruments ) pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyotumika wakati wa upasuaji huo (Consumables ) kutoka kwa timu ya wataalam wa afya wa nchini Japan , Mkuruenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema zoezi hilo la upasuaji litafanyika kesho na keshokutwa .
‘’Tumekua na ushirikiano mzuri na wataalam hawa kwa muda wa miaka 12 sasa na niamini ushirikiano huu utaendelea, lakini pia uwepo wa Madaktari hawa utusaidia kuwajengea uwezo watalaam wetu hapa Muhimbili,” . Amesema Profesa Museru.
Profesa Museru amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo MNH ina mahitaji ya vifaa mbalimbali vya vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa .
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na MNH katika kuboresha huduma za afya na kudumisha ushirikinao huo wa kihistoria.
Hivyo makala 30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili
yaani makala yote 30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/30-kufanyiwa-upasuaji-wa-mtoto-wa-jicho_12.html
0 Response to "30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili"
Post a Comment