title : Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi
kiungo : Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi
Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi
Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu muda mchache baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.
Kioo cha gari kikionyesha sehemu iliyipita risasi
Waziri huyo kijana aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia kwani alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.
Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri.
Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.Hivyo makala Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi
yaani makala yote Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/waziri-kijana-zaidi-wa-somalia-auawa.html
0 Response to "Waziri kijana zaidi wa Somalia auawa kwa risasi"
Post a Comment