title : Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego
kiungo : Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego
Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo ‘Wapo’ kwaajili ya Rais John Pombe Magufuli iko tayari na inaweza kuachiwa muda wowote.
Rapa Nay wa Mitego
Rais Magufuli aliufungulia ‘original version’ ya wimbo huo baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na kumtaka rapa, Nay wa Mitego kuongeza baadhi ya maneno katika wimbo huo ili uwaguse watu wengi zaidi.
Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo huo iko tayari na ameongeza vitu ngingi ndani ya wimbo huo.
“Kusema kweli wimbo wa Mh Rais umekamilika na muda wowote unaweza kutoka,” alisema Nay. “Nimeongeza mambo mengi ndani yake, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya moto mwingine kwa sababu bado ‘Wopo’ yenyewe inaendelea kufanya vizuri,”
Rapa huyo amedai hawezi kusema ni lini project hiyo itatoka.
Katika hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumuunga mkono katika muziki wake pamoja na kujitokeza kwa wingi katika tour yake ya ‘Wapo’ ambayo imeingia ndani ya jiji la Dar es salaam.
Hivyo makala Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego
yaani makala yote Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/remix-ya-wimbo-wapo-ya-rais-magufuli.html
0 Response to "Remix ya wimbo ‘Wapo’ ya Rais Magufuli iko tayari – Nay wa Mitego"
Post a Comment